Watendaji Wakuu na Wataalam Sekta ya Afya SADC wakutana.

Ukanda wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC, umeonesha maendeleo chanya katika vita dhidi ya kifua kikuu, UKIMWI, Malaria pamoja na huduma za lishe.

Takwimu zinaonyesha kati ya mwaka 2015 na 2018 vifo vilivyotokana na maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu vilipungua kwa asilimia 15, kesi mpya za malaria zikipungua kwa asilimia 24 huku maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa watu wenye umri wa miaka 15 na kuendelea yakipungua kwa asilimia 27 mwaka 2010 hadi 2018.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam katika mkutano wa kisekta wa watendaji wakuu na wataalamu wa sekta ya afya na UKIMWI kutoka nchi wanachama wa SADC, unaotangulia mkutano wa mawaziri wa nchi za SADC wa sekta hiyo.

Mwenyekiti wa mkutano huo katibu mkuu kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Zainabu Chaula anasema umelenga kuangalia hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa itifaki ya Afya ya SADC ya mwaka 1999 na mpango mkakati wa kanda kuhusu masuala ya Afya pamoja na kuridhia maazimio kuhusu masuala hayo ambayo yatajadiliwa katika mkutano huu.

Naye Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko amesema elimu zaidi inahitajika ili kuendelea kudhibiti maambukizi mapya ya vvu, pamoja na kuweka juhudi za pamoja.

Mkutano huu una takribani ajenda 13, ikiwa ni pamoja na mijadala ya magonjwa yanayoambukiza na kuathiri nchi za SADC ukiwa na kauli mbiu isemayo Ushirikiano wa nchi za SADC ni nguzo kuu kufikia Maendeleo Endelevu ya sekta ya afya ambapo Tanzania ina fursa ya kuwa msambazaji wa dawa katika nchi za SADC.

Mkutano huu ni mwendelezo wa mikutano ya kisekta ya SADC takribani 50 itakayofanyika nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja, kufuatia Tanzania kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo hadi mwezi Agosti 2020.

Comments

comments

clement

Read Previous

Mvutano kati ya Salva Kiir na Riek Machar wazua wasiwasi.

Read Next

Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!