Iran kupunguza ahadi zake za mkataba wa Nyuklia.

Iran imesema itachukua hatua mpya katika kupunguza ahadi ilizotoa katika mkataba wa kihistoria wa nyuklia wa 2015 kuanzia kesho Jumatano kwa kuongeza gesi kwenye mitambo yake 1,044 ya urutubishaji Uranium katika kiwanda chake cha Fordow.

Katika hotuba yake kupitia televisheni, Rais Hassan Rouhani amesema hatua hiyo ni majibu ya moja kwa moja kwa rais wa Marekani Donald Trump ya kuiondoa Marekani katika makubaliano ya nyuklia yaliotiwa saini mwaka 2015 ambayo yaliiruhusu Iran kuongeza viwango vya kurutubisha madini ya Uranium bila kuongeza gesi kinyume na tangazo lililotolewa na Rouhani.

Mapema jana Iran ilizindua mitambo aina ya 30 IR-6 ya kurutubisha madini ya Uranium na kwa sasa taifa hilo lina mitambo 60 ya kisasa hali inayoashiria azma ya nchi hiyo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Miaka minne ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Read Next

Mafanikio miaka minne ya Rais Magufuli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!