Ziara ya Katibu mkuu wa CCM siku ya pili Kisiwani Mafia.

Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally, leo amehitimisha ziara yake ya siku mbili kisiwani Mafia, na kusisitiza maana halisi ya CCM Mpya ambapo haimaanishi kubadili katiba ila upya wa sasa ni utaratibu Mpya wa Mhe. Rais na Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt. John Pombe Magufuli wa kusema na kutenda pamoja kuhakikisha misingi ya usawa na haki inaimarishwa zaidi.

Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally ametoa kauli hiyo katika Mkutano wake wa ndani na kata nne za Kilindoni, Miburani, Kiegeani na Jibondo Kisiwani Mafia ambao umehudhuriwa na wanachama wa CCM, viongozi wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa Pwani Ramadhani Maneno na Mbunge wa Mafia Mbaraka Dau.

Awali Katibu Mkuu wa CCM Dkt. BASHIRU ALLY alikagua maendeleo ya ukarabati wa Hospitali ya wilaya ya Mafia na ujenzi wa Gati ya kisasa katika kisiwa hicho.

Naye Mbunge wa Mafia Mbaraka Dau ametumia fursa hiyo kuishukuru serikali ya CCM kwa kuendelea kusambaza umeme katika vijiji vyote vya jimbo hilo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Uvujaji wa gesi Kilwa.

Read Next

Wafanyabiashara mikoa ya kaskazini wavutiwa na Bandari ya Tanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!