Uvujaji wa gesi Kilwa.

Hali ya upatikanaji wa nishati ya gesi katika kituo cha kupokea nishati hiyo Somanga Mtama kitongoji cha njia nne wilayani Kilwa mkoani Lindi imerejea kama kawaida kufuatia jitihada za marekebisho zilizofanywa na wataalam wa ndani na nje.

Hitilafu iliyotokea ilisababisha kukosekana kwa nishati ya gesi kwenye kituo hicho pamoja na taharuki kwa baadhi ya wakazi na wasafiri wa barabara kuu ya Mtwara Lindi Dar es salaam kwa saa kadhaa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa mwishoni mwa wiki hali iliyozua taharuki na kuathiri huduma mbalimbali ikiwemo usafiri kwa zaidi ya saa 7 pamoja na uzalishaji wa umeme. Usafirishaji wa gesi umerejea tena baada ya marekebisho ya siku tatu mfululizo ambapo Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) limesema kazi ya kufua umeme itarejea kama kawaida.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dkt. Tito Mwinuka amewaambia waandishi wa habari hali ilivyo mara baada ya kukagua kituo cha kupokea Gesi toka Songosongo kinachomilikiwa na kampuni ya SONGAS kilichosimama kutokana na kuvuja kwa gesi na kulazimika kuzima mitambo.

Meneja wa Utafiti Mafuta na Gesi toka shirika la maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC) Venosa Ngowi, akielezea kuhusu taharuki iliyotokea kutokana na hitilafu hiyo amebainisha kuwa pamoja na hali hiyo gesi inayozalishwa ni salama kwa asilimia kubwa huku baadhi ya wakazi wa Somanga wakiomba kupatiwa elimu ya kutosha ili kuondoa hofu kutokana na uwepo wa nishati hiyo umbali mfupi na makazi yao.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Wanasayansi watahadharisha kuhusu mabadiliko ya Tabianchi.

Read Next

Ziara ya Katibu mkuu wa CCM siku ya pili Kisiwani Mafia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!