Mafanikio miaka minne ya Rais Magufuli.

Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli imeweza kutekeleza miradi mbalimbali yenye manufaa kwa wananchi katika kipindi kifupi cha miaka minne kutokana na kuweka usimamizi mzuri wa mapato ya serikali na kuelekeza fedha nyingi zaidi katika huduma za jamii.

Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Dkt.Hassan Abbas amebainisha hayo jijini Dar es salaam katika mkutano wa waandishi wa habari uliolenga kuleta tafakuri ya wanahabari kuhusu miaka minne ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Dkt.Hassan Abbas amesisitiza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano katika azma yake ya kujitegemea imesimamia mapato ya Serikali na kupiga vita rushwa na ubadhirifu ili mapato hayo yatumike katika maeneo yanayostahiki.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Iran kupunguza ahadi zake za mkataba wa Nyuklia.

Read Next

Wanasayansi watahadharisha kuhusu mabadiliko ya Tabianchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!