Wafanyabiashara mikoa ya kaskazini wavutiwa na Bandari ya Tanga.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imefanikiwa kuwarudisha wafanyabiashara wa mikoa ya kanda ya kaskazini ambao walikuwa wanatumia bandari ya nchi jirani kushusha mizigo yao kutoka nje ya nchi ambapo sasa wameanza kutumia bandari ya Tanga baada ya bandari hiyo kufanyiwa maboresho makubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea bandari ya Tanga kuona maboresho makubwa yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano ikiwemo ya uchimbaji wa kina cha bahari katika mlango wa kuingilia bandarini hapo, mkurugenzi mkuu wa TPA Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema kuwa katika kipindi cha mwaka jana wafanyabiashara wa mikoa ya kanda ya kaskazini walitumia bandari ya nchi jirani kushusha tani laki mbili na hamsini ambapo kwa mwaka huu tani laki moja tayari zimeshushwa katika bandari ya tanga.

Aidha akizungumzia mapato ya bandari ya Tanga, meneja wa bandari hiyo Ajuaye Msese amesema kuwa serikali imefanikiwa kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 20 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019 kutoka bilioni 14 za mwaka 2017/2018.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Ziara ya Katibu mkuu wa CCM siku ya pili Kisiwani Mafia.

Read Next

Uzinduzi wa mikopo kwa wajasiriamali wadogo Kigamboni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!