Uzinduzi wa mikopo kwa wajasiriamali wadogo Kigamboni.

Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es salaam imezindua mikopo kwa wajasiriamali wadogo kupitia benki ya CRDB ijulikanayo kama (Jiwezeshe) ambapo jumla ya shilingi bilioni 10 zimetengwa kwa ajili ya wajasiriamali 3,400 wenye vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Desemba mwaka jana ambao wamekidhi vigezo wakitarajiwa kupata mikopo hiyo ambayo itatolewa kwa njia ya kidigitali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mikopo hiyo Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Josephat Kandege amesema inaelekea kutimiza azma ya Mhe. Rais Magufuli ya kukuza mitaji ya wajasiriamali na kuwa walipaji wakubwa wa kodi ambapo ametumia fursa hiyo kuziagiza Halmashauri zote nchini kutumia kigezo cha kitambulisho cha mjasiriamali kama kipaumbele cha kwanza kwa makundi maalumu yanayostahili kupata mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani inayotengwa na Halmashauri hizo.

Aidha amesisitiza kuwa mikopo hiyo inayotolewa kwa wanawake, vijana na walemavu imekuwa ikitolewa bila kuwa na ufuatiliaji wa kutosha huku akisisitiza kuwa fedha hizo si za kugawa bure bali zinatakiwa kurejeshwa ili ziweze kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Akizungumzia mikopo hiyo ambayo imetajwa ni ya kwanza kutolewa Tanzania nzima mkuu wa wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri amesema lengo la mikopo hiyo ni kukipa thamani kitambulisho cha mjasiriamali na kuwainua wajasiriamali kwa kukuza biashara zao ambapo watakopeshwa katika makundi matatu ambayo itatolewa kwa masharti nafuu.

Mkurugenzi mtendaji Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela amesema baada ya kuona mkakati wa serikali wa kuwainua wajasiriamali benki hiyo imeamua kuunga mkono juhudi hizo kwa kuhakikisha kundi hili lenye mchango mkubwa katika usambazaji wa bidhaa kwa walaji kutoka viwandani linapata mikopo kwa njia rahisi ambayo itatolewa bila dhamana bali wanatakiwa kuwa kitambulisho cha mjasiriamali na wawe wamejiunga na huduma za kibenki kwa njia ya kidigitali.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Wafanyabiashara mikoa ya kaskazini wavutiwa na Bandari ya Tanga.

Read Next

China kununua Korosho Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram