Wanasayansi watahadharisha kuhusu mabadiliko ya Tabianchi.

Wanasayansi wameonya kuwa mabadiliko ya tabia nchi yanaweza hivi karibuni kufikia katika kiwango ambacho hakiwezi kubadilishwa tena.

Wakati hali hiyo ikiendelea kuwa isiyoeleweka, kuna makubaliano juu ya njia bora za kuzuia hali hiyo isifikiwe, ambayo ni kupunguza kwa haraka utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira.

Njia ya msingi ya kufanikisha upunguzaji wa utoaji gesi chafu, ni utekelezwaji wa makubaliano ya mazingira ya Paris ya mwaka 2015 yaliyolenga kubakiza nyuzi joto mbili juu ya viwango vilivyokuwepo kabla ya mapinduzi ya viwanda ambayo hata hivyo yanaonekana hayatoshi.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya mfuko wa kuhifadhi mfumo wa ikolojia, UEF, takribani asilimia 75 ya ahadi katika makubaliano ya Paris nchini Ufaransa yameamuliwa bila kutosha katika kupunguza kasi ya mabadiliko ya tabia nchi na ahadi hizo bado hazijatekelezwa.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mafanikio miaka minne ya Rais Magufuli.

Read Next

Uvujaji wa gesi Kilwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!