Halmashauri ya Kilombero yahamishwa.

Wananchi wa halmashauri mpya ya Mlimba mkoani Morogoro wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuridhia halmashauri ya Kilombero kuhamia Mlimba wakionyesha matumaini kuwa ujio wa halmashauri hiyo utachochea kasi ya maendeleo katika eneo lao.

Wakiongea na mkuu wa wilaya ya Kilombero James Ihunyo baada ya kukagua majengo na eneo itakapojengwa Halmashuri ya Mlimba na kumkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri Stephano Kaliwa, wananchi wa eneo hilo wamesema kuwa uwepo wa halmashauri hiyo utasaidia kukuza uchumi wao na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa kuwa changamoto ya kutembea mwendo mrefu itapungua huku Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Kilombero Clarence Mgomba amesema eneo hilo ni zuri na lina nyumba za kuanzia makazi na ofisi.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilombero Jamsi Ihunyo amewataka watumishi wote kuhamia haraka iwezekanavyo ili kuwasaidia wananchi wa halmashauri hiyo mpya na kuongeza kuwa makazi ya kuishi katika eneo hilo ni rafiki kwa watumishi huku mkurugenzi wa Halmashauri hiyo mpya Stephano Kaliwa amepokea majengo hayo na kukiri kuwa ni mazuri.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

China kununua Korosho Tanzania.

Read Next

TANZANITE kuhakikishiwa soko la madini duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram