China kununua Korosho Tanzania.

Jamhuri ya watu wa China inaangalia uwezekano wa kuongeza uwekezaji katika zao la korosho ikiwemo kununua korosho yote ambayo inalimwa hapa Tanzania ambapo kwa kuanzia wawekezaji kutoka nchi hiyo tayari wamewekeza kiwanda cha kubagua korosho mkoani Mtwara.

Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke amefafanua katika maonyesho ya kimataifa ya kibiashara yanayoendelea hivi sasa mjini Shangai ambapo rais wa China Xi Jinping mbali na kuwepo kwa mabanda mengi kutoka nchi mbalimbali Afrika ametembelea banda la pekee la Tanzania kuangalia uzalishaji wa korosho huku akitoa rai kuboreshwa kwa sera ili wawekezaji wajitokeze wengi zaidi kutoka mataifa mengine.

Balozi Wang Ke amesema hayo wakati akiwa ziarani mkoani Morogoro na kukagua utendaji wa kituo cha maonyesho ya teknolojia ya kilimo cha kichina kilichopo wilayani Mvomero.

Awali wadau walioalikwa katika gafla hiyo wamepongeza kuwepo kwa kituo hicho ambacho kimesaidia wakulima na watafiti katika uzalishaji wenye tija.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Uzinduzi wa mikopo kwa wajasiriamali wadogo Kigamboni.

Read Next

Halmashauri ya Kilombero yahamishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!