TANZANITE kuhakikishiwa soko la madini duniani.

Wafanyabiashara wakubwa wa madini duniani wameihakikishia Tanzania kupatikana kwa soko la kudumu la madini ya Tanzaniate duniani, jambo ambalo linatoa uhakika wa soko na kupanda kwa thamani ya madini hayo.

Waziri wa Madini Dotto Biteko ameyasema hayo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, katika hafla ya kuwaaga wafanyabishara wa madini ya Tanzanite kutoka Marekani, waliokuwa nchini kwa siku tano kujifunza na kuimarisha mahusiano kuhusu biashara ya madini hayo.

Biteko Amesema anautazama ujio wafanyabishara hawa wakubwa wa Tanzaniate duniani, kama sehemu muhimu ya kuitangaza Tanzanite ya Tanzania kimataifa.

Aidha, Biteko ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wachimbaji na wafanyabiashara wa Tanzanite nchini kupitia chama chao TAMIDA kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa maslahi ya taifa.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Halmashauri ya Kilombero yahamishwa.

Read Next

Uchunguzi dhidi ya Rais Trump kuanza Novemba 13.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!