Uchunguzi dhidi ya Rais Trump kuanza Novemba 13.

Wabunge wa Chama cha Democrats wametangaza kuanza kwa mahojiano ya wazi wiki ijayo katika uchunguzi ambao unaweza kushuhudia Rais wa Marekani Donald Trump akiondolewa madarakani.

Taarifa yao imeonyesha kuwa maofisa watatu wa juu kutoka wizara ya mambo ya nje watatoa ushahidi, baada ya kuwa wamehojiwa kwa siri kwa wiki kadhaa.

Uchunguzi unaofanywa na wabunge umejikita katika madai kuwa rais Trump alimshinikiza rais wa Ukraine kutangaza hadharani uchunguzi dhidi ya mpinzani wake Joe Biden wakati wa kugombea urais.

Mwenyekiti wa kamati ya Intelijensia, Adam Schiff ambaye anasimamia mchakato huu, amewaambia waandishi wa habari kuwa taratibu zote zimekamilika ambapo pia wamechapisha nyaraka za mahojiano waliyofanya na mashahidi watakaoitwa. Hata hivyo Rais Trump amekosoa mchakato huu ulioanzishwa na Chama cha Democrats akisema hakuna kosa alilofanya wakati wa maongezi yake na rais wa Ukraine, kauli inayoungwa mkono na baadhi ya wabunge wa chama chake.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

TANZANITE kuhakikishiwa soko la madini duniani.

Read Next

Mkutano wa Mawaziri sekta ya Afya na Ukimwi nchi za SADC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram