Mnada wa Kwanza wa Korosho Lindi.

Wakulima wa Korosho wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi chini ya chama kikuu cha Runali wameridhia kuuza korosho zao kwa bei ya shilingi 2625 na 2567 kwa kila kilo ambapo jumla Maombi 20 ya kampuni 15 za ununuzi yalijitokeza katika mnada huo ukiwa ni wa kwanza kufanyika mkoani humo kwa msimu huu.

Katika Mnada huo uliohudhuriwa na wakulima, Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, Jumla ya tani 438 kati ya tani 3442 zilizoombwa na makampuni ziliuzwa baada mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ruangwa Nachingwea na Liwale (RUNALI) kuwahoji na kuridhia.

Awali Kaimu Mrajis wa Ushirika Mkoa wa Lindi Robert Nsunza kupitia hadhara hiyo alisimamia mnada wa uwazi kwa wanunuzi na wakulima na baadaye kutangaza washindi huku Kaimu Mkurugenzi wa bodi ya korosho Tanzania, Francis Alfred akitoa msisitizo wa malipo kwa msimu huu wa 2019/2020.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Rais Dkt. Magufuli amesisitiza ushirikiano Kiuchumi nchi za Afrika.

Read Next

Mikopo ya Elimu ya Juu yafikia Tsh. Bilioni 162.8 .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!