Rais Dkt. Magufuli amesisitiza ushirikiano Kiuchumi nchi za Afrika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amesisitiza haja ya kuwepo ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi za Kiafrika na zile za Nordic kupitia diplomasia ya uchumi badala ya kuendeleza ushirikiano wa zamani wa nchi zinazotoa misaada na zile zinazopokea misaada.

Mhe.Rais Magufuli ametoa wito huo leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akifungua rasmi mkutano wa 18 wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Afrika na Nordic ambao unafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania na kuhudhuriwa na zaidi ya nchi 42.

Aidha, Mhe.Rais Magufuli amebainisha kwamba katika mazingira ya sasa ya ulimwengu, lazima mwelekeo wa ushirikiano baina ya Afrika na nchi za Nordic ubadilike ili uendane na mazingira yaliyopo ambapo amesema bara la Afrika limejaaliwa maliasili na rasilimali nyingi zinazohitaji kuendelezwa na Waafrika wenyewe.

Comments

comments

clement

Read Previous

Mkutano wa Mawaziri sekta ya Afya na Ukimwi nchi za SADC.

Read Next

Mnada wa Kwanza wa Korosho Lindi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!