Umoja wa Mataifa wataka Mazungumzo Nchini Bolivia.

Maafisa wa Bolivia wamesema Umoja wa Mataifa umeitolea mwito serikali ya nchi hiyo, kuanzisha mazungumzo kwa lengo la kusuluhisha mzozo baina ya Rais wa mpito, Jeanine Anez na wafuasi wa Rais aliyejiuzulu na kukikimbia nchi Evo Morales.

Tayari watu 23 wamekwishapoteza maisha kutokana na mzozo huo, na nchi hiyo ya Amerika Kusini hivi sasa inakabiliwa na upungufu wa chakula.

Bi. Jeaninne Anez alijitangaza kuwa Rais wa Mpito wa Bolivia baada ya Rais Morales kujiuzulu na kukimbilia Mexico tarehe 10 Novemba kufuatia shinikizo kubwa la maandamano dhidi yake.

Comments

comments

clement

Read Previous

Waziri Mkuu awasimamisha kazi Wakurugenzi watatu.

Read Next

Wakazi wa Tegeta waishukuru Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram