Shambulio la kigaidi nchini Mali laua Askari 24.

Jeshi la Mali limeshambuliwa na kundi la watu wanaoshukiwa kuwa magaidi Kaskazini mwa nchi hiyo karibu na mpaka wa Niger na kuua Askari zaidi ya 24 huku raia wengi wakipoteza maisha katika shambulio hilo lililotokea jana Jumatatu Novemba 18.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la nchi hiyo imeeleza kuwa Washambuliaji wa tukio hilo ambao walionekana kujiandaa kikamilifu kutekeleza mauaji hayo walikuwa kwenye gari saba na pikipiki zikiwemo pikipiki za matairi matatu ambazo ni mali ya kituo kimoja cha Afya ambapo magaidi 17 waliweza kuuawa na Askari wa Libya na kufanikiwa kuharibu vifaa mbalimbali vya Magaidi hao.

Jeshi la Mali limeeleza kuwa Kikosi cha askari walioshambuliwa walikuwa wakienda kujiunga na vikosi vya jeshi la Niger kwenye operesheni ya pamoja inayofanywa na Vikosi vya Askari kutoka nchi hizo mbili inayoitwa Tongo Tongo karibu na mpaka unaozitenganisha nchi hizo mbili.

Mapigano hayo yalitokea katika mji wa MÈnaka. Askari wa Mali waliojeruhiwa walipokelewa nchini Niger.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Wakazi wa Tegeta waishukuru Serikali.

Read Next

Rais Dkt. Magufuli apokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Ramaphosa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram