Watu wawili wafariki kwa Ajali, Tisa wajeruhiwa Mbeya.

Watu wawili ambao ni raia wa Nchini Malawi na Ethiopia wamefariki dunia huku wengine tisa wanaodhaniwa kuwa ni raia wa Ethiopia wakiwa wamejeruhiwa, baada ya lori walilokuwa wakisafiria kwa njia isiyo halali kuelekea nchini Malawi kupinduka katika kijiji cha Namba One Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Akizungumzia ajali hii Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulirich Matei amesema watu hao ambao ni Raia kutoka Nchini Ethiopia walitokea nchini Kenya na kupitia Mpaka wa Namanga , wakielekea Lilongwe Nchini Malawi , Kamanda Matei anasema raia hao wa Ethiopia walihifadhiwa uvunguni mwa gari kwenye Cheses katika gari lenye namba za usajili CA 6439 lenye tela namba BK 4744 aina ya Genlyon mali ya Kampuni ya Almedia ya Nchini Malawi , ambapo iliacha njia na kupinduka na kusababaisha kifo cha dereva aliyefahamika kwa jina la George Kamanga ambaye ni raia wa Nchini Malawi.

Majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Makandanda ambayo ni Hospitali ya Wilaya ya Rungwe na kwamba hali zao zinaendelea vizuri .

Comments

comments

clement

Read Previous

Meya wa Jiji la Arusha Kalist Lazaro ahamia CCM.

Read Next

TAKUKURU yawafikisha raia 2 wa China.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram