Watu wawili wauawa katika shambulizi Damascus.

Watu wawili wameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa na Israeli katika mji mkuu wa Syria, Damascus.

Awali msemaji wa jeshi la Israeli Avichay Adraee alisema kuwa Israeli ilishambulia maeneo yaliyolengwa ya jeshi la Iran na Syria nchini humo kama hatua ya kulipiza kisasi kwa makombora yaliyorushwa kuelekea nchini Israeli siku moja kabla.

Shirika la habari la serikali nchini Syria, SANA, limesema jeshi la ulinzi la anga la Syria lilifanikiwa kuharibu baadhi ya makombora yaliyorushwa na ndege za Israeli kabla ya kufikia maeneo yaliolengwa.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Jamii yaombwa kutoa taarifa za Matukio ya Ukatili.

Read Next

Serikali yazitaka Taasisi za Fedha kufika Vijijini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram