China haitokubali Hong Kong kuhujumiwa.

China imepinga hatua ya wabunge wa Marekani kuidhinisha miswada miwili ya kuunga mkono juhudi za kudai Demokrasia ndani ya Hong Kong.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, amesema China haitomruhusu mtu yoyote kuharibu ustawi na utulivu wa Hong Kong.

Muswada mmoja unatoa nafasi ya kuwekewa vikwazo maafisa wa China na Hong Kong wanaokiuka haki za binadamu pamoja na kufanyiwa mapitio ya kila mwaka hadhi maalum ya kibiashara iliyotolewa na Marekani kwa mji wa Hong Kong na mwingine unapiga marufuku mauzo ya silaha kwa polisi wa Hong Kong ikiwemo mabomu ya kutoa machozi, risasi za mpira na magari ya maji ya kuwasha.

China imeieleza Marekani kwamba haitokubali mfumo wa Nchi Moja Serikali Mbili kuhujumiwa.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Uzinduzi wa Ushirikiano Kati ya Bodi ya Utalii na NAS.

Read Next

Bunge kubadili kanuni za Utambulisho wa Wabunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram