Bunge kubadili kanuni za Utambulisho wa Wabunge.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linakusudia kubadilisha kanuni zake zinazotambulisha wabunge wa Chama Tawala na Vyama vya Upinzani, ili kuondoa dhana ya wabunge wa upinzani kuwa kazi yao ni kupinga tu.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, BW. JOB NDUGAI, wakati alipokuwa akifunga bunge la sita la vijana, lililokaa kwa muda siku saba.

Aidha, Spika huyo wa Bunge akachukua fursa hiyo kutoa shukrani kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kwa uamuzi wake wa kulipa jina soko kuu jipya la Dodoma, jina la JOB NDUGAI.

Mapema akimkaribisha kufunga bunge hilo, Spika wa Bunge la Vijana BW. RAMADHANI SINGA, akauomba uongozi wa bunge kufikiria kuongeza idadi ya wabunge wa bunge hilo la vijana, huku siku wakiomba pia siku ziongezwe, ili waweze kujifunza kwa undani zaidi, jinsi ya uendeshaji wa shuguli za bunge.

Comments

comments

clement

Read Previous

China haitokubali Hong Kong kuhujumiwa.

Read Next

Waziri Mkuu ahimiza umuhimu wa kufanya Ibada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram