Muungano wa Vyama Tawala Ethiopia waunda Chama Kimoja.

Muungano wa vyama tawala nchini Ethiopia umeidhinisha hatua ya kuungana kwa vyama vinne vilivyo katika misingi ya kikabila kuwa chama kimoja cha kitaifa kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo mwaka 2020, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Waziri Mkuu Abiy Ahmed kuleta umoja, licha ya chama kimoja kususia mkutano huo na upigaji wa kura.

Abiy amesema uamuzi huo wa kuunganisha vyama umechukuliwa kwa pamoja, wakati wajumbe waliopinga muungano huo hawakuwapo katika chumba cha mkutano.

Waziri mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed amesema chama hicho kipya kina lengo la kuimarisha na kutekeleza mfumo halisi wa majimbo ambao unatambua tofauti na michango ya raia wa Ethiopia.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Waziri Mkuu ahimiza umuhimu wa kufanya Ibada.

Read Next

Rais Dkt. Magufuli aweka mawe ya msingi ya Ujenzi wa Miradi ya Maendeleo Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!