Rais Dkt. Magufuli aweka mawe ya msingi ya Ujenzi wa Miradi ya Maendeleo Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. JOHN POMBE MAGUFULI leo ameweka mawe ya Msingi katika Ujenzi wa Miradi Mbalimbali yenye hadhi ya jiji la Dodoma, ikiwamo mradi wa kituo kikuu cha mabasi, nyumba za askari polisi, Hospitali ya Uhuru pamoja na soko la kisasa alilolipa jina la NDUGAI.

Akizindua Nyumba za makazi ya Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU Rais Magufuli akawataka askari wenye vyeo vya juu waache kuwanyanyasa walio chini yao, na kwamba askari hao wanapaswa kuachwa Wafanye kazi zao kwa Mujibu wa Sheria Bila kuingiliwa na viongozi wao wa Juu ili waweze kutenda haki.

Kwa upande wake Inspekta Jenerali wa Polisi Nchini IGP SIMON SIRRO akaelezea kupungua kwa matendo ya uhalifu ya makosa ya jinai kwa asilimia 24.9, unyangíanyi wa kutumia nguvu kwa asilimia 54.2 na makosa ya barabarani kwa asilimia 69.4 kwa kipindi cha miaka minne iliyopita huku waziri wa mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola akiyataja mafanikio hayo kuwa sehemu ya uongozi bora wa Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine Rais Dkt. Magufuli akaelezea kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa hospitali ya Uhuru wilayani Chamwino pamoja na soko la kisasa na stendi ya mabasi na kuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Dodoma kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati.

Comments

comments

clement

Read Previous

Muungano wa Vyama Tawala Ethiopia waunda Chama Kimoja.

Read Next

Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa Kesho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram