Waziri Mkuu ahimiza umuhimu wa kufanya Ibada.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema licha ya majukumu mengi waliyonayo wananchi, wanatakiwa kutambua kuwa suala la kufanya ibada ni jambo muhimu, hivyo hawana budi kulitekeleza.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu baada ya kumalizika kwa sala ya Ijumaa katika msikiti wa Gaddaf jijini Dodoma.

Amesema badala ya kuwaacha watoto kucheza ni wajibu wa wazazi na walezi kuwahimiza kwenda msikitini pindi wakati unapowadia lengo kuwajenga kwenye misingi imara ya kiimani na makuzi yaliyo bora.

Awali, Waziri Mkuu alizungumzia kuhusu ushirikiano uliopo baina ya viongozi wa dini na Serikali, ambapo amesema Serikali inafarijika sana na ushirikiano huo unaoifanya iendelee kuliongoza Taifa kwa mujimbu wa imani walizonazo wananchi.

Comments

comments

clement

Read Previous

Bunge kubadili kanuni za Utambulisho wa Wabunge.

Read Next

Muungano wa Vyama Tawala Ethiopia waunda Chama Kimoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram