Ndege isiyo ya rubani ya Marekani kupotea Libya.

Jeshi la Marekani limesema kuwa limepoteza ndege isiyoendeshwa na rubani ambayo haikuwa na ulinzi katika mji mkuu wa Libya, Tripoli ambapo makundi hasimu yamekuwa yakipigania udhibiti wa mji huo kwa miezi kadhaa sasa.

Uongozi wa kijeshi wa Marekani barani Afrika – AFRICOM umesema kuwa ndege hiyo isiyokuwa na Rubani ilipotea ilipokuwa ikikadiria hali ya usalama na kufuatilia shughuli za makundi hayo yenye itikadi kali.

Kikosi hicho cha AFRICOM hakikutoa sababu ya kupotea kwa ndege hiyo kwa kuwa bado kinafanya uchunguzi. Hata hivyo kikosi hicho kimeongeza kuwa operesheni za ndege zisizokuwa na marubani nchini Libya, zimeshirikishwa vyema na maafisa wakuu wa Serikali wanaostahili.

Tangu mwaka 2015, Libya inatawaliwa na Serikali mbili, moja ikiwa na makao yake mjini Tripoli na nyingine katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo. Vikosi vya kijeshi vinavyoiunga mkono serikali ya Mashariki vimekuwa vikijaribu kuchukuwa udhibiti wa mji huo mkuu tangu mwezi Aprili.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Ujenzi wa Meli mpya Mwanza kukamilika kwa wakati.

Read Next

Serikali yapokea gawio lenye thamani ya Tshs. Trilioni 1.05 .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram