Sidama, Ethiopia wachagua kujisimamia.

Tume ya uchaguzi nchini Ethiopia imesema kabila la Sidama kupitia kura ya maoni iliyopigwa wiki iliyopita wameamua kuwa na Serikali ya kimkoa kwa asilimia 98.5, wakati makundi mengi ya kikabila yakidai uhuru zaidi.

Matokeo hayo yanaupa Mkoa wa Sidama ambao unawakilisha asilimia 4 ya idadi ya watu milioni 105 wa Ethiopia, haki ya kujiongoza, ambapo kwa sasa utakuwa wa 10 na utakuwa na mamlaka ya kukusanya kodi, kusimamia elimu, usalama na baadhi ya Sheria.

Katiba ya Nchi hiyo inatoa haki ya kudai uhuru kwa makundi zaidi ya 80 ya kikabila, ikiwa ni chini ya mageuzi ya kisiasa ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed ambapo watu wa Sidama wameweza kupiga kura.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Waliokaidi agizo la kususia Uchaguzi waeleza.

Read Next

Walioshinda Serikali za Mitaa Waapishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram