TRA yafanikiwa kuongeza mapato.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kuongeza mapato ya serikali kwa miaka minne mfululizo hivyo kufanya jumla ya Mapato yote kuwa shilingi za Kitanzania trilioni 58.3 ikilinganishwa na trilioni 38.97 katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo amebainisha hayo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizungumzia mafanikio ya TRA katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, ambapo amesema yanatokana na msukumo wa serikali kuendelea kuboresha mikakati ya kuimarisha ukusanyaji wa mapato, kuibua vyanzo vipya vya kodi pamoja na utekelezaji wa mpango mkakati wa tano wa TRA wa ukusanyaji kodi wenye dhamira ya kuongeza makusanyo ya kodi za ndani kwa kukuza ulipaji kodi kwa hiari.

Naibu Kamishna huyo pia amezungumzia mafanikio katika kuongeza Idadi ya walipa kodi kutoka milioni mbili na laki mbili mwaka 2015/16 hadi kufikia milioni tatu na elfu kumi kwa takwimu za Oktoba 2019 kufuatia kuwepo kwa Serikali sikivu.

Amesema licha ya mafanikio hayo TRA pia imekabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukwepaji kodi wa makusudi na Biashara za magendo. Hapa Naibu Kamishna Mbibo anatoa Wito kwa wafanyabiashara na jamii kwa ujumla.

Mafanikio ya TRA pia yamewezeshwa na kuimarika kwa matumizi ya mashine za EFD, ongezeko la mizigo kutoka nje ya nchi kupitia bandari Dsm pamoja na kuboreshwa kwa mifumo.

Comments

comments

clement

Read Previous

Walioshinda Serikali za Mitaa Waapishwa.

Read Next

Vyuo Vikuu na vya Kati kuongezewa uwezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram