Vyuo Vikuu na vya Kati kuongezewa uwezo.

Vyuo Vikuu na vya Kati hapa nchini vitaongezewa uwezo wa kudahili zaidi wanafunzi, hatua ambayo inatarajiwa kuongeza ufanisi wa vijana pindi wanapoingia kwenye soko la ajira hapa nchini na Ukanda wa Afrika Mashariki.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Leonard Akwilapo amebainisha hayo wakati alipokuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano la siku nne linalojumuisha wasomi kutoka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki za Tanzania, Kenya na Ethiopia.

Amesema mpango huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa gharama ya Dola Milioni 75 ambazo zitatumika kuviongezea uwezo vyuo vya ufundi vya hapa nchini vya DIT kampasi ya Dsm na Mwanza, Chuo cha Ufundi Arusha na Chuo cha NIT ambapo matarajio ni kuwa wahitimu watakuwa na uwezo wa kutenda kazi mara wamalizapo vyuo badala ya kusubiri kupata uzoefu.

Comments

comments

clement

Read Previous

TRA yafanikiwa kuongeza mapato.

Read Next

Ujenzi wa Rada Mbeya wakamilika kwa zaidi ya Asilimia 65.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram