Walioshinda Serikali za Mitaa Waapishwa.

Msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Tarime mjini Bi. Janeth Tungu kwa kushirikiana na hakimu mkazi wa Mahakama ya Mwanzo wamewaapisha viongozi 486 wa Chama cha Mapinduzi waliopita bila kupingwa huku chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kikiambulia wajumbe wawili kati ya vitongoji 508 katika wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Baada ya kutangaza idadi ya viongozi waliopita bila kupingwa wa Chama cha Mapinduzi Tarime mjini Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Mhe. Mitembe Chana amewaaapisha viongozi hao huku mkurugenzi mtendaji wa mji wa Tarime Bw. Elius Mtiungwa akiwataka viongozi wateule kwenda kusimamia miradi ya maendeleo ya jamii inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tarime Bw. Daud Ngicho amewataka viongozi wa Serikali za Mitaa kuacha tabia ya kutembea na mihuri kwenye mifuko na badala yake wafanye kazi kwa uadilifu mkubwa kwa niaba ya chama tawala.

Comments

comments

clement

Read Previous

Sidama, Ethiopia wachagua kujisimamia.

Read Next

TRA yafanikiwa kuongeza mapato.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram