Bodi ya filamu Imewakumbusha wamiliki wa Vyombo vya Usafiri na Wasimamizi hasa magari ya abiria kuacha tabia ya kuonyesha filamu au picha jongevu ambazo hazina maadili kwa Watanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo amesema Hatua kali za kisheria zitakuchukuliwa kwa wale wote watakaokaidi agizo hilo ikiwemo kulipa faini ya shilingi Milioni 1 au kupelekwa mahakamani.
Katika hatua nyingine amevitaka vyombo vya Usafiri hasa vya abiria kuhakikisha picha jongevu zote watakazotaka kuzionyesha katika Vyombo vya usafiri ziwe na kibali kutoka Bodi ya filamu Tanzania.
Naye Mwanasheria wa wizara ya habari Evod Kyando amesema wamiliki wa vyombo vya moto au wasimamizi wanaowajibu wa kuhakikisha filamu,Video za Muziki au Picha Jongevu zinakidhi vigezo vya sheria ya Bodi ya Filamu pamoja na kanuni zake.