Dkt. Bashiru awatahadharisha wabunge/wawakilishi.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ali amewatahadharisha baadhi ya wabunge na wawakilishi wa chama hicho wanaoacha kutekeleza majukumu yao yanayotokana na ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 – 2020.

Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Bashiru Ali ameyasema hayo wakati akizungumza na wazee pamoja na wastaafu ofisi kuu ya CCM Kisiwandui mara baada ya kupata malalamiko ya wazee hao kufuatia uwepo wa baadhi ya wabunge na wawakilishi kujipendekeza kwa wapiga kura badala ya kufanya mambo kwa maslahi mapana ya chama na taifa kwa ujumla.

Amesema CCM haitahangaika na walalahoi wanaojitafutia maslahi bali chama kitachagua mgombea kikiangalia utekelezwaji wa ilani kwa lengo la kuwatumikia wananchi.

Aidha Dkt. Bashiru anasema mfumo pekee wakuepusha makundi na mipasuko ni utaratibu wa kikatiba ambao ndio muongozo wakusimamia masuala yote ndani ya Chama cha Mapinduzi.

Mapema Dkt. Bashiru Ali alipata fursa yakutembelea kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar hayati Abeid Amani Karume nakumuombea dua ikiwa ni ishara ya upendo kwa yale aliyoyaanzisha katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Comments

comments

clement

Read Previous

TAKUKURU wakabidhiwa ripoti ya ubadhirifu.

Read Next

Rais Magufuli mgeni rasmi siku ya Uhuru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram