Idadi ya waliokufa kwa mafuriko Kenya yafikia 65.

Maafisa nchini Kenya wamesema idadi ya waliokufa kutokana na athari za mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo tangu Jumamosi ya wiki iliyopita imeongezeka na kufikia 65 baada ya mvua kubwa kuendelea kunyesha hapo jana na kuua watu wengine watano kwenye eneo la Bonde la Ufa.

Mkuu wa polisi wa eneo la Kajiado, Daudi Loronyokwe amesema watu hao watano ikiwemo watoto watatu walikuwa wakirejea nyumbani baada ya kushiriki dhifa ya harusi nchini Tanzania wakati gari lao liliposombwa na maji.

Gavana John Lonyang’apuo amesema kati ya watu 80,000 na 120,000 wameathirika kwenye kaunti ya Pokot Magharibi, eneo lililokumbwa zaidi na mafuriko pamoja na mapormoko ya udongo yaliyowauwa watu 52

Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limesema juhudi za uokozi zinaendelea lakini limeonya kuwa sehemu kadhaa za nchi hiyo zitaendelea kukumbwa na mafuriko makubwa ndani ya wiki hii.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Watu Nane washikiliwa, Sita wanatafutwa.

Read Next

Bodi ya filamu yatoa rai kwa wamiliki vya vyombo vya usafiri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!