Wananchi Namibia wapiga kura kuwachagua viongozi.

Upigaji kura umeanza leo nchini Namibia katika uchaguzi wa rais na wabunge ambapo hali ngumu ya maisha na kashfa za rushwa zinaweza kuwa changamoto kwa chama tawala.

Taifa hilo lenye wakazi wachache, limekuwa likitawaliwa na chama cha South West Africa Peoples Organisation (SWAPO) tangu nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1990.

Rais Hage Geingob ambaye anawania kuchaguliwa tena baada ya muhula wake wa kwanza ameelezea kujiamini kuwa atashinda, lakini atakubali matokeo endapo atashindwa kwa kuwa yeye ni muumini wa demokrasia.

Hata hivyo Rais huyo, anakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa Panduleni Itula mmoja wa vigogo wa chama cha Swapo aliyejitenga.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Serikali yaagiza PSSSF kushusha bei za nyumba.

Read Next

Halmashauri na Mikopo ya Biashara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram