Watoa huduma za Afya dhidi ya Ebola wauawa DRC.

Shirika la Afya duniani WHO limesema kundi lenye silaha limeuwa watoa huduma za afya watatu na wengine wanne kujeruhiwa katika jimbo la Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuonya kuwa kitendo hicho kinaweza kukwamisha jitihada za kuutokomeza ugonjwa huo ambazo zilianza kupata mafanikio.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanon Ghebreyesus kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kwamba walichokuwa wakihofia kimetokea.

Tukio hili linatokea siku chache baada ya hali ya machafuko kuukumba mji wa Beni, ambako wakazi walivamia kituo cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Kongo, MONUSCO, kuushinikiza ujumbe huo kufanya juhudi zaidi kuhakiksha usalama wa raia.

WHO imewahamisha wafanyakazi wake wapatao 49, na kuwabakisha 71 katika eneo hilo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mkuu wa Mkoa Mbeya atoa siku 17.

Read Next

Uzinduzi wa Msikiti wa Haq.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram