Mkuu wa Mkoa Mbeya atoa siku 17.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amempa siku 17 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mbeya, awe amekata maji kwa taasisi zote za serikali ambazo zinadaiwa ankra za maji na kusababisha deni kufikia shilingi bilioni 1.85 kati ya shilingi billion 4.9 ya deni lote ambalo linahusisha wateja mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila ametoa maamuzi haya baada ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mbeya kuwasilisha taarifa kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa akieleza Taasisi za Serikali kuwa na deni kubwa la ankra za maji.

Channel ten imefanya mahojiano na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mhandisi Ndele Mengo ambapo amezitaja baadhi ya Taasisi hizo kuwa ni Jeshi la Polisi na Magereza ambazo zinadaiwa zaidi ya shilingi milioni 600 na kwamba madeni hayo yamekuwa yakikwamisha utendaji wa kazi wa Mamlaka hiyo hasa kwa miradi ambayo inatumia fedha za ndani.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Uzinduzi wa Bima ya Afya NHIF.

Read Next

Watoa huduma za Afya dhidi ya Ebola wauawa DRC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram