Uzinduzi wa Bima ya Afya NHIF.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya – NHIF umezindua rasmi mpango mpya wa uchangiaji wa huduma za afya kwa kutumia vifurushi mbalimbali kulingana na uwezo wa mtu lengo likiwa ni kuhakikisha kila mtanzania anatibiwa kwa kutumia bima ya afya.

Akizungumza kabla ya kuzindua mpango huo ambao ulienda sambamba na ugawaji wa kadi kwa wananchi waliojiandikisha katika mpango huo Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Spika Mstaafu Anna Makinda ametoa rai kwa watoa huduma za afya hususan katika vituo vya afya na hospitali za serikali kutoa huduma zinazostahili kwa wagonjwa ili kutekeleza kwa vitendo Ilani ya chama cha Mapinduzi katika sekta ya Afya.

Aidha amewataka Watanzania kuondoa dhana kwamba kujiunga na huduma za bima ya afya usipotibiwa kwa mwaka ni hasara bali ni mtindo wa kuchangiana kwa mzunguko na kumwezesha kila mwanachama kupata matibabu pindi anapougua.

Wakizungumzia mfumo huo baadhi ya wakazi wa jiji la DSM ambao wamekabidhiwa kadi zao kupitia vifurushi hivyo vipya wamesema imetoa fursa kwa kila Mtanzania kupata huduma hiyo kulingana na uwezo wake hivyo imerahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu wakati wowote na mahali popote.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Serikali yasisitiza mifumo imara ya Takwimu.

Read Next

Mkuu wa Mkoa Mbeya atoa siku 17.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram