Uzinduzi wa Msikiti wa Haq.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amesema amani na utulivu iliopo nchini umechangiwa kwa kiasi kikubwa na Taasisi za Dini ambazo zimekuwa zikiwajenga waumini wao katika Misingi ya kumjua Mwenyezi Mungu ikiwemo uadilifu na Utii ambapo amezitaka Taasisi hizo kuongeza nguvu ili kuwapata Viongozi bora wa Baadaye.

Akizungumza katika hafla ya ya Uzinduzi wa Msikiti wa Kisasa wa Masjid Haq Uliopo Mtaa wa Kionga Magomeni Mapipa jijini Dsm, Mhe. Majaliwa amesema Viongozi wa Dini wamekuwa na Mchango mkubwa katika kutoa nasaha zenye kuwajenga waumini wao katika maadili na matendo mema ambapo amesisitiza kuendelea na kazi hiyo kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Mwakilishi wa Mufti wa Tanzania ambaye pia ni Imam wa Msikiti wa Manyema Sheikh Masoud Jongo akizungumza kwa niaba ya Mufti amewataka Viongozi wa Dini kuendelea kuiunga mkono Serikali katika jitihada zake za kuwaletea Maendeleo wananchi.

Katika Kuchangia Ujenzi wa Msikiti huo Upande wa Akina Mama ambao haujakamilika Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli alichangia Shilingi Milioni 10, Mhe. Waziri Mkuu alichangia Shilingi Milioni 5 Huku viongozi mbali mbali akiwemo Waziri wa Ulinzi Dkt. Husein Mwinyi, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega nao pia walichangia Ujenzi wa Msikiti huo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Watoa huduma za Afya dhidi ya Ebola wauawa DRC.

Read Next

Waziri Jaffo aunda kamati ya uchunguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!