Hospitali ya Muhimbili yazindua wodi mbili za Watoto.

Hospitali ya Taifa Muhimbili imefanikiwa kuzindua wodi mbili za watoto wanaohitaji uangalizi maalum ikiwa ni mageuzi makubwa yanayoendelea kufanyika katika uboreshaji wa huduma katika hospitali hiyo.

Akizungumza katika ufunguzi huo mwenyekiti wa bodi ya Muhimbili, Profesa Charles Majinge, amesema kwa kipindi kirefu watoto katika hospitali ya taifa muhimbili walikuwa hawana ICU maalum hivyo kulazwa ICU za watu wazima hali iliyosababisha watoto hao kukosa huduma muhimu.

Amesema kwa uzinduzi wa ICU hizi mbili hususan kwa watoto wachanga kuanzia umri wa siku sifuri hadi 28 almaarufu NICU na watoto kuanzia siku 29 hadi miaka 14 PICU ni ukombozi mkubwa katika kuendeleza mafanikio ya kupunguza idadi ya vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano ambapo tayari Tanzania ikiwa moja ya nchi zilizofanikiwa kwa theluthi mbili.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya taifa Muhimbili Dkt. Hedwiga Swai amesema hospitali hiyo imefanikiwa kupunguza vifo vya watoto wachanga kutoka asilimia 19.2 mwaka 2017/18 mpaka asilimia 16.2 mwaka 2018/19.

Hata hivyo kaimu mkurugenzi Dkt. Swai anasema licha ya mafanikio haya wanakabiliwa na changamoto za vifaa, mafunzo na huduma ili ICU hizi ziweze kutoa huduma kwa ufanisi.

Hospitali ya taifa Muhimbili ilipata msaada kutoka kwa mke wa mfalme wa Sharja wa Falme za Kiarabu kupitia shirika la Tumaini la Maisha wa kufanya ukarabati na kuwekewa vifaa vya kisasa wodi mbili za watoto wachanga na watoto wasiozidi miaka 14 wenye uhitaji wa uangalizi maalum kwa gharama ya shilingi za Kitanzania bilioni 4.9.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Waziri Jaffo aunda kamati ya uchunguzi.

Read Next

Uzinduzi wa kampeni ya Soko kwa Soko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram