Uzinduzi wa kampeni ya Soko kwa Soko.

Radio Magic Fm inayomilikiwa na kampuni ya Afrika Media Group Limited ambao pia ni wamiliki wa Channel ten, wamezindua kampeni maalumu ya Soko kwa Soko kupitia kipindi cha Morning Magic kinachorushwa na Radio hiyo ambapo kwa mara ya kwanza uzinduzi huo umefanyiaka katika soko la Kisutu Jijini Dar es salaam na wafanyabiashara wa soko hilo pamoja na waendesha bodaboda kujipatia zawadi mbalimbali.

Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanywa na Mstahiki Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto ambaye ameonyesha kufurahishwa na kampeni hiyo ambayo licha ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo lakini pia kampeni hiyo itaisaidia Serikali kujua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara.

Awali, Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Radio Magic FM Lazaro Matalange, Mkurugenzi wa masoko wa Africa Media Group Limited Aman Nicolas na Mtangazaji wa kipindi cha Morning Magic Orest Kawau wamesema lengo la kampeni hiyo ni kuwakusanya wafanyabiashara wadogo na kuwakutanisha na wafanyabiashara wakubwa.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Hospitali ya Muhimbili yazindua wodi mbili za Watoto.

Read Next

Sudan yakifuta chama tawala cha Al-Bashir.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!