Sudan yakifuta chama tawala cha Al-Bashir.

Utawala mpya wa Sudan umeamuru kuwa chama cha kiongozi wa kiimla aliyeondolewa madarakani Omar al-Bashir kivunjwe na utawala wake “usambaratishwe” ukiitikia mwito wa waandamanaji ambao kampeni yao ilisababisha kuangushwa kwa kiongozi hiyo.

Bashir na chama chake cha National Congress – NCP aliiongoza nchi hiyo ya Afrika Kaskazini tangu mwaka wa 1989 kabla ya vuguvugu la maandamano ya kitaifa kumuondoa madarakani mapema mwaka huu.

Baraza jipya la uongozi nchini humo na baraza la Mawaziri likiongozwa na Waziri Mkuu Abdalla Hamdok limefanya uamuzi wa kukivunja chama kwa kuidhinisha sheria iliyoitwa “kuusambaratisha utawala wa Juni 30 1989.”

Amesema kamati itaundwa ili kukamata mali zote za chama hicho. Waziri Mkuu huyo amesema hatua hiyo sio kulipiza kisasi dhidi ya watawala wa zamani wa nchi hiyo, bali ni kudumisha hadhi ya watu wa Sudan ambayo ilichafuliwa na watu wasio wakweli.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Uzinduzi wa kampeni ya Soko kwa Soko.

Read Next

IGP Sirro awaonya wanaondelea kuwanyanyasa Wanawake na Watoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!