Waziri Jaffo aunda kamati ya uchunguzi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jaffo ameunda Kamati ya Uchunguzi katika Ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha Kisasa cha Mbezi jijini Dsm ili kubaini uwepo wa ukiukaji wa taratibu za ukandarasi zikiwemo kubadilisha Michoro baada ya kupata taarifa zilizoonyesha kuwapo kwa kutoelewana kati ya Msimamizi Mshauri wa mradi na Mkurugenzi wa jiji la Dsm.

Akizungumza baada ya kufanya ziara ya Ukaguzi wa Mradi huo wa ujenzi wa stendi ya Kisasa unaogharimu kiasi cha Bilioni 50.9 amesema pamoja na kazi nzuri iliyofanyika ya ujenzi wa Stendi hiyo lakini pia akaendelea kusisitiza Ubora kwa kuwa fedha zinazotumika ni za walipa kodi wa Tanzania.

Awali Mkurugenzi wa Jiji la Dsm Siporah Liana ambaye ndio msimamizi Mkuu wa Mradi wa Ujenzi huo mkubwa amesema amekuwa akipambana na vikwazo hasa kutoka kwa Mkandarasi Mshauri kutokana na Usimamizi wake makini ambapo mpaka sasa mradi umekamilika kwa asilimia 50 lakini fedha alizolipa ni bilioni 9 badala ya bilion 24 .

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Uzinduzi wa Msikiti wa Haq.

Read Next

Hospitali ya Muhimbili yazindua wodi mbili za Watoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram