IGP Sirro awaonya wanaondelea kuwanyanyasa Wanawake na Watoto.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro ameendelea kuwaonya watu wanaonyanyasa wanawake na watoto kwa kuwasababishia vipigo na ukatili wa aina nyingine ambao ni kinyume cha sheria za nchi.

IGP Sirro amesema hayo jana wakati akizindua Ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto wilayani Bunda mkoa wa Mara, ujenzi uliofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani UNFPA pamoja na Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto yaani CDF.

Katika sherehe hizo za uzinduzi zilizohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mwalimu Lydia Bupilipili, IGP Sirro amewataka wananchi kutumia ofisi hiyo ya Dawati la Kijinsia na Watoto ili kukomesha vitendo vya ukatili sambamba na kuwataka wazazi kuwaendeleza kielimu watoto wao jambo ambalo litasaidia jamii kuwa na viongozi bora.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Sudan yakifuta chama tawala cha Al-Bashir.

Read Next

Watumishi wa Afya watakiwa kueleza umuhimu wa dawa za kufifisha Virusi vya Ukimwi, ARV.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!