Watumishi wa Afya watakiwa kueleza umuhimu wa dawa za kufifisha Virusi vya Ukimwi, ARV.

Watumishi wa sekta ya afya katika Halmashauri za Wilaya mkoani Tanga wametakiwa kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuendelea kutumia dawa za ARV’s na kuwapima wingi wa Virusi vilivyopo mwilini mwao mara kwa mara.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Isaya Mbenje kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika kimkoa katika wilaya ya Pangani.

Katika kila watu mia moja watu watano wana maambukizi ya Virusi vya UKIMWI mkoani hapa na kuonyesha kuwa hali ya maambukizi bado ni kubwa kutokana na takwimu zilizopo.

Na hapa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Pangani akawataka watumishi wa Idara ya Afya kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wateja wao.

Rose Kiluvia ni Kaimu Mratibu wa VVU Mkoa wa Tanga yeye akaelezea moja ya changamoto wanayokutana nayo kwenye kazi zao huku Dkt. Anastazia Masanja ambae ni Afisa Mradi kutoka kampeni ya furaha yangu akielezea namna wanayotekeleza majukumu yao.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wakaishauri jamii juu ya kupima afya zao mapema ili wajitambue.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

IGP Sirro awaonya wanaondelea kuwanyanyasa Wanawake na Watoto.

Read Next

Waziri Lukuvi amvua cheo Mkuu wa Idara ya Ardhi Manispaa ya Iringa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!