Dodoma kuanzisha Mahakama maalum kwa wanaoharibu mazingira.

Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma umesema upo katika mchakato wa kuunda sheria ndogo chini ya sheria ya mazingira zitakazoshinikiza wananchi kutunza mazingira kwa kupanda miti huku watakaokiuka watafikishwa katika mahakama ya jiji itakayoanzishwa hivi karibuni.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Halmashuri ya Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi wakati wa uzinduzi wa msimu wa upandaji miti katika jiji hili ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan la kila halmashauri ihakikishe inapanda angalau miti zaidi ya milioni 1.5 kwa mwaka.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Partobas Katambi akaagiza wakala wa huduma za misitu nchini TFS wahakikishe wanaandaa miche ya miti kwa ajili ya taasisi ikiwamo vyuo vikuu, vya kati na mashirika ya Serikali.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Dodoma ya Kijani kupitia TFS Yohana Sanga anafafanua utaratibu unaotumika na mamlaka ya jiji ili kuidhinisha ramani ya ujenzi kwa wanaoomba vibali ambapo wanatoa kipaumbele kwa wanaobainisha sehemu za kupanda miti.

Hadi kufikia mwezi Novemba mwaka huu zaidi ya miti laki sita imepandwa katika jiji la Dodoma ambapo katika msimu unaoanza sasa TFS kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania Foundation, shirika la wanyamapori WWF na ofisi ya Makamu wa Rais wanakusudia kupanda miti mingine zaidi ya laki tisa.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Waziri Lukuvi amvua cheo Mkuu wa Idara ya Ardhi Manispaa ya Iringa.

Read Next

Raia na waumini wa Kanisa la Kiprotestant wanaomboleza vifo vya waumini 14 waliouawa jana wakati wa Ibada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!