Waziri Lukuvi amvua cheo Mkuu wa Idara ya Ardhi Manispaa ya Iringa.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amechukua hatua za kinidhamu kwa kumuondoa katika nafasi yake ya kazi Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Wilbert Mtongani baada ya kubaini amefungua ofisi yake binafsi ambayo inashughulikia masuala ya ardhi, kiasi cha kumfanya apoteze muda mwingi wa kazi katika ofisi hiyo na kuisababishia halmashauri hiyo kukosa mapato yake.

Akiongea katika mkutano wa hadhara ambao lengo lake ni kupokea kero za ardhi katika mkoa wa Iringa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema amelazimika kuchukua hatua hiyo baada ya kuona mtumishi huyo anachukua muda wote wa kazi katika ofisi yake binafsi na kuwatoza wananchi kiasi kikubwa cha pesa kwa kushughulikia matatizo yao ya ardhi jambo ambalo limekuwa likiikosesha Manispaa hiyo maduhuli yake halali.

Awali akimkaribisha Waziri Lukuvi, Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amesema ofisi yake kwa kushirikiana na wataalamu imekuwa na utaratibu wa kudumu wa kushughulikia Migogoro ya Ardhi.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Watumishi wa Afya watakiwa kueleza umuhimu wa dawa za kufifisha Virusi vya Ukimwi, ARV.

Read Next

Dodoma kuanzisha Mahakama maalum kwa wanaoharibu mazingira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!