Raia na waumini wa Kanisa la Kiprotestant wanaomboleza vifo vya waumini 14 waliouawa jana wakati wa Ibada.

Raia nchini Burkina Faso na waumini wa madhehebu ya Kiprotestant wanaomboleza vifo vya waumini 14 waliouawa Jumapili wakati wa ibada katika mji wa Hantoukoura, mashariki mwa Burkina Faso baada ya kuvamiwa na watu waliojihami kwa silaha na kufanya mashambulizi hayo ya kikatili.

Makundi ya kijihadi yamenyooshewa kidole cha lawama kwamba yanaendelea kuhatarisha usalama katika sehemu za ibada.

Vitendo vya makundi ya kijihadi kushambulia sehemu za ibada vimekuwa vikiongezeka kila mara huko nchini Burkina Faso na kwa mujibu wa chanzo cha usalama kilichonukuliwa na Shirika la Habari la AFP shambulio hilo liliendeshwa na watu waliojihami kwa silaha za kivita.

Vikosi vya ulinzi na usalama vimeanza kutoa msaada kwa watu waliojeruhiwa.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Dodoma kuanzisha Mahakama maalum kwa wanaoharibu mazingira.

Read Next

Ukaguzi wa magari yanayoingiza Korosho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!