Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linasema, limewauwa waasi zaidi ya 80 wa ADF katika wilaya ya Beni, katika operesheni dhidi ya makundi ya waasi.

Hii ni operesheni inayokuja baada ya waasi hao kuendelea na mauaji ya raia zaidi ya 100 tangu Novemba, katika Wilaya hiyo na kuzua wasiwasi kuhusu usalama wa wakaazi wa Beni.

Wananchi Mashariki mwa nchi hiyo wameendelea kuandamana kulaani kutokuwepo uhakika wa usalama, wakishinikiza kuondoka kwa jeshi la Umoja wa Mataifa MONUSCO kwa kile wanachosema, limeshindwa kuwalinda raia hao.

Hivi karibuni Rais Felix Tshisekedi Tshilombo aliapa kuyatokomeza makundi yanayohatarisha usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikiwa ni pamoja na kundi hili la waasi wa Uganda la ADF.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

TRA yajikita kupanua wigo wa walipakodi nchini.

Read Next

Serikali Kahama yatambua maeneo ya uchimbaji Madini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram