Ukaguzi wa magari yanayoingiza Korosho.

Kufuatia uingizaji wa korosho ghafi zisizo na ubora kutoka mkoa wa Pwani ili ziuzwe katika minada inayoendelea mkoani Lindi kinyume na utaratibu, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imejipanga kuanza ukaguzi katika magari yanayoingia na kutoka ili kudhibiti uingizaji huo haramu unaoathiri bei za korosho wilayani humo.

Akizungumza na Channel Ten mara baada ya kufunga kikao cha robo ya pili cha baraza la madiwani Wilaya ya Kilwa, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Abuu Mussa Mjaka amebainisha kuwa uwepo wa uingizaji wa korosho hizo katika maghala yaliyo mipakani kunachangia kuathiri bei na kukosesha mapato ya Mkulima na Wilaya.

Kutokana na hali hiyo tayari mipango ya udhibiti imeanza kupitia vizuizi mbalimbali ikiwemo njia za bahari kama inavyobainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Abuu Mussa Mjaka na Baadhi ya Madiwani wa kata mbalimbali.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Raia na waumini wa Kanisa la Kiprotestant wanaomboleza vifo vya waumini 14 waliouawa jana wakati wa Ibada.

Read Next

Mafuriko yaikumba Babati na kukosesha Kaya 426 makazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram