Utafiti elimu ya mafunzo ya ufundi stadi.

Serikali imeombwa kuangalia namna ya kuboresha mitaala ya elimu ya mafunzo ya ufundi stadi nchini ili yaweze kuisadia Tanzania kufikia dhamira ya uchumi wa viwanda.

Sambamba na hilo imetakiwa kuwe na ukaguzi wa kuhakikisha vyuo vinavyotoa elimu hiyo vinakuwa na vifaa na vitendea kazi vya kisasa na vya kutosha na kuboresha usimamizi wa vyuo hivyo ili viweze kuleta tija iliyokusudiwa.

Rai hiyo imetolewa katika mapendekezo ya utafiti ulioangalia tatizo la ajira kwa vijana wanaomaliza elimu ya mafunzo ya ufundi stadi na kusaka ajira, iliyofanywa na taasisi ya utafiti ya REPOA ambayo imeonesha elimu ya ufundi stadi ikiboreshwa ina uwezo wa kutoa wahitimu watakaokuwa na uwezo wa kuisadia Tanzania kufikia uchumi wa viwanda kwa kutoa taaluma inayohitajika viwandani na kwingineko.

Nao washiriki kutoka vyuo vya elimu ya juu na watendaji kutoka taasisi mbalimbali wameongeza pia umuhimu wa kuangaliwa upya kwa utaratibu wa vigezo vya kuingia katika elimu ya mafunzo ya ufundi stadi nchini pamoja na namna ya kupata mikopo ya kununua vifaa vya kazi ili kuweza kujiajiri.

Utafiti umefanyika ndani ya miaka miwili ukilenga kuangalia tatizo la ajira kwa vijana wanaomaliza elimu ya mafunzo ya ufundi stadi na kubaini changamoto kadhaa, ikiwemo wingi wa vijana kuingia kwenye elimu hiyo wakiwa na elimu ndogo, elimu inayotolewa kutokidhi mahitaji ya soko la ajira, vitendea kazi vyuoni kutokidhi mahitaji kamili kutokana na wingi wa wanafunzi na idadi ya waalimu kuwa ndogo kulinganisha na idadi ya wanafunzi huku mgawanyo wa vyuo hivyo kutokuwa na usawa nchini.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Wafanyabiashara ya madini kutoa taarifa kwa mtandao.

Read Next

UN: Watu milioni 168 watahitaji msaada wa kibinadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram