Wafanyabiashara ya madini kutoa taarifa kwa mtandao.

Serikali kupitia Wizara ya Madini inaanzisha mfumo wa kimtandao ambao wafanyabiashara wa madini wataweza kuwasilisha kiwango cha madini walichonacho hata kabla ya kufika sokoni ili kuwezesha serikali kupata mapato stahili kutokana na rasilimali hiyo ya nchi.

Mpango wa kuwa na mfumo huo umetangazwa jijini Dodoma na Waziri wa Madini Bw. Dotto Biteko wakati alipokuwa akiwapokea watumishi wapya wa madini, vifaa na vitendea kazi mbalimbali vitakavyowezesha sekta hiyo iweze kufikia makusanyo ya shilingi bilioni 470 katika mwaka huu wa fedha.

Aidha, Waziri huyo wa madini akachukua wasaa huo kuwaasa watumishi wapya kuja kutekeleza wajibu wao wa kuwatumikia Watanzania kwa kuzisimamia rasilimali zao ili ziweze kuwasaidia na siyo kujihusisha na vitendo vya wizi na udanganyifu kwa ajili ya tamaa katika utumishi wao.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ya Madini Prof. Simon Msanjila akawakumbusha juu ya deni kubwa walilonalo baada ya kupokea vifaa hivyo vya kuboresha utendaji wao wa kazi.

Katika hafla hiyo fupi, jumla ya watumishi wapya 166 walipokelewa ikiwa ni hatua ya kuongeza ufanisi katika usimamizi wa sekta ya madini nchini.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mafuriko ya mvua yaathiri baadhi ya maeneo ya Tabora.

Read Next

Utafiti elimu ya mafunzo ya ufundi stadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram