Serikali Kahama yatambua maeneo ya uchimbaji Madini.

Serikali kupitia Wizara ya Madini, Wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeanza utaratibu wa kuwatambua na kuwapangia maeneo ya kufanya shughuli za uchimbaji na maeneo ya viwanda vidogo vya kutengeneza malighafi zinazotokana na madini ya ujenzi kama kokoto, mchanga, mawe na changalawe kwa lengo la kuhakikisha eneo hilo linashiriki kikamilifu katika kulipa kodi ya serikali iliyopo kwa mujibu wa sheria.

Afisa madini mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Joseph Kumburu anafika na kukagua moja ya eneo la kuponda kokoto, mjini kahama. Kinachofanyika hapa katika eneo hili ni kupewa elimu dhidi ya tozo na kodi za serikali zinazotozwa na sekta ya madini ya ujenzi.

Kufuatia kuwepo kwa ukwepaji wa kodi inayotokana na madini ya ujenzi, ofisi ya madini mkoa wa Shinyanga inawakutanisha wadau wa sekta hiyo katika mkutano wa pamoja kwa lengo la kutoa elimu na miongozo mbalimbali ya serikali na hapa waainisha changamoto zao. Sekta ya Madini imejielekeza kukusanya kutokana na madini ya ujenzi.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Read Next

Maonyesho ya Utalii karibuni Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram